
Udaftari uliochapisha maarifa nchini Canada
Mwingilio Mkuu
Kunyanyaswa si mazuri katika kila lugha
Main entry under title:
Abuse
is wrong in any language
Umetolewa pia kwa lugha ya Kifaransa chini ya kichwa:
La violence est inacceptable peu
importe la langue
ISBN 978-0-662-03029-4
Cat. no J2-131/2008Sw
HV6626.23C3A38 1995 362.829’2’0971 C95-980093-X
Huu ni mradi ya Umma unaoshugulikia Elimu ya Sheria na Habari chini ya Idara inayoshugulikia Uhasama katika jamii
Imehadhiriwa kwa mamlaka ya Waziri wa haki na Wakili Mkuu Wa Canada
kwa
Idara ya Haki nchini Canada
Ottawa, Ontario
K1A 0H8
© Wizara ya Kazi ya Umma na Huduma nchini Canada 2008
Imechapishwa nchini Canada
Umekubaliwa kunakili kitabu hiki bila ruhusa kutoka kwa idara ya Sheria bora tu umetambua kwamba chanzo cha kitabu hiki kimezingatiwa. Ikiwa umepanga kutimia habari hii kwenye fomati tofauti na jinsi ilivyo, ni muhimu upate barua ya ruhusa kutoka kwa idara.
(Swahili)
Idara ya Sheria inashukuru huduma ya kuelimisha sheria kwa raia na kituo cha mawasiliano cha New Brunswick kwa kuturuhusu kutumia utungo la chapisho lao kama asili ya kitabu hiki.
Idara ya sheria pia inaungama mchango ya mtandao wa PLEI wafanyikazi katika idara ya Haki na Sheria na Wakili Mkuu; Idara Uraia na Uhamiaji nchini Canada; Idara ya Urithi na Tamaduni Canada; Idara ya Afya; Hakimu Mkuu wa Canada; pamoja na Idara ya Hadhi ya Wanawake nchini Canada. (majina ya idara yameandikwa kulingana na wakati wa kuchapishwa)
Kijitabu hiki kilitayarishwa baada ya mazungumzo baina ya vikundi mbali mbali vya kitamaduni na vya jumuia zilizoko nchini Canada. Tunawapa shukrani kwa wale wote waliosaidia na tunawashukuru kwa kuchangia kwenye harakati huu muhimu.
Kijitabu hiki ni cha wanawake waliohamia au wakimbizi wanaoteseka kwa kunyanyaswa kwenye mahusiano au familia yao. Ukijua mtu yeyote anayenyanyaswa tafadhali mpe kijitabu hiki. Muulize kama anahitaji usaidizi. Pengine anaweza kukutegemea. Mjulishe kwamba hayupo pekee yake.
Ijapokuwa kijitabu hiki kimeandikwa kwa mujibu ya wanawake wahamiaji na wakimbizi, vile vile sio vizuri kwa mwanaume anyanyaswe. Basi mtu yeyote anayenyanyaswa anaombwa kutafuta usaidizi.
Kama mwanmke aliyehama au mkimbizi unaweza kuhisi kwamba upo pekee yako. Unaweza kuwa na shida ya kuzungumza na watu. Ikiwa unanyanyaswa, unaweza kuhofia wewe mwenyewe pamoja na watoto wako.
Itakubidi ujue zaidi sheria za nchi ya Canada, haki zako pamoja na aina ya usaidizi ambayo unaweza kupata unaponyanyaswa.
Piga simu kwa polisi au kwa rafiki ikiwezekana.
Kimbia nje ili watu wakuone (isipokuwas unafikiria kwamba utakuwa salama ndani ya nyumba).
Piga mayowe – Wjulishe majirani ili kwamba wakaiti polisi.
Umenyanyaswa ikiwa mtu mwingine amekuumiza au kukutendea vibaya.
Unyanyasaji unaweza kuwa wa kimwili, wa ugoni, wa hisia, saikolojia au wa kifedha. Unaweza kunyanyaswa kwa zaidi ya moja ya haya.
Mara nyingi, mwenye kukunyanyasa ni mume wako au mke wako, mume au mke wa zamani. Wakati mwingine ni mmoja wa jamii yako, au jamii ya mke/mume wako, au jamii ya mume/mke wako wa zamani. Anaweza kuwa ni mtu wa kike au mwanamume.
Mifano wa kudhulumiwa kwa mwili ni kama yafuatayo:
Hizi mfano wa hujumu ni hatia nchini Canada.
Manyanyaso ya kimapenzi ni mapenzi ya kushikwashikwa au mapenzi ya kutendeka kabla haujakubaliana nayo.
Hi pia ni hatia nchini Canada.
Matukano ya hisia au ya kisaikolojia yaweza kuzingatiwa:
Haya ni hatia nchini Canada.
Baadhi ya mfano za kunyanyaswa kifedha ni:
Haya ni hatia nchini Canada.
Minyanyaso zingine zinazowezekana sio hatia lakini bado ni uovu na hakuna mtu yeyote mwenye haki ya kukutendea maovu haya. Baadhi ya mfano haya ni:
Kuna watu wanaweza kukusaidia.
Piga simu kwa jumuiya ya mashirika za kitamaduni zinazowatumikia wahamiaji au wakimbizi. Uliza ni nini wanaweza kufanya ili kukusaidia. Waulize kama wanajua mahali pengine ambapo unaweza kupata usaidizi.
Piga simu kwa polisi. Watakulinda pamoja na watoto wako.
Unaweza pia kupata usaidizi
Pia, unaweza kupata usaidizi ikiwa umeamua utaendelea kukaa papo hapo.
Unyanyasaji hufanyika kwa jamii ya aina mbali mbali. Hufanyika kwa wanainchi wa Canada na kwa wahamiaji. Inafanyika kwa wanawake walio na watoto pamoja na wale hawana watoto, kwa matajiri na masikini, kwa wataalamu na wamama wanaokaa nyumbani, kwa vijana na kwa wazee. Hufanyika kwa wanawake wote watu mbali mbali pasipochagua dini, utaifa, utamaduni, au kabila. Unyanyasaji unaweza kufanyika katika hatua yoyote ya mahusiano.
Kuongea juu ya kunyanyaswa unaweza kuwa ni jambo magumu. Wanawake wengi walionyanyaswa wana haya au wanaogopa kwamba familia na marafiki hawatawaamini. Lakini, kumbuka – hakuna chochote ufanyayo inayompa mtu yeyote ruhusa ya kukunyanyasa. Hakuna sababu kamwe ya kunyanyasa mtu. Na sio hatia yako.
Wanawake wengi wamegundua kwamba kuna mviringo ya kunyanyaswa. Mvutano unajijenga kwa muda fulani hadi anayenyanyasa anaanza kukudhulumu. Baada ya “timko” au kudhulumiwa, kuna wakati wa kimya au umakini. Baadaye anaweza kusema kwamba anasikitika na kusema pole hata kuahidi kwamba halitafanyika tena. Hata hivyo, kupitia wakati, mvutano unaanza na yeye hufanya madhulumu kwako tena. Hivyo basi mviringo wa kunyanyaswa huendelea.

Ni jambo gumu sana kwa watoto kuona au kisikia mzazi wao ananyanyaswa. Inaweza kuathiri vitendo vyao, afya na akili yao, kujiheshimu binafsi, na hata utendaji wa masomo yao. Inaweza pia kuathiri maingiano kati ya mtoto na wengine. Vijana wanaoshuhudia unyanyasaji manyumbani kwao yamkini huendelea kunyanyasa wake zao wakisha kuwa watu wazima. Wasichana nao yamkini wanakubaliana na unyanyasaji kama kitu cha kawaida katika maisha ya uhusiano baina ya watu waliooana.
Kama mzazi anyeteswa, inaweza kuwa vigumu kwako kuwatunza watoto wako. Watoto wanaweza kujifunza kumtazama anayekunyanyasa hivyo basi kukosa kukuheshimu. Unyanyasaji unaweza pia kukumaliza pumzi mpaka ukose nguvu za kugawanya na watoto wako.
Ikiwa mwenye ananyanyasa pia anawanyanyasa watoto, ni vyema upate usaidizi kwa niaba ya watoto. Kunyanyasa watoto pia ni hatia dhidi ya sheria. Unaweza kuenda kwa kituo cha maslahi ya watoto au huduma ya jamii ili upate ushauri na usaidizi zaidi. Watoto wanahitajika kulindwa kutokana na unyanyasaji.
Kwanza, ni muhimu ufikiri juu ya usalama yako pamoja na watoto wako. Unaweza kuhofia kwamba jamii yako pamoja na marafiki wako hawatakusaidia ikiwa umeondoka. Hi yaweza kufanyika. Hata hivyo, itakuwa vyema kwako na watoto wako kuliko kuendelea kunyanyaswa.
Unaweza kuondoka kwa muda mfupi au kwa kudumu. Walakini, haimaanishi kwamba umekata kauli ya ndoa yako au umevunja mahusiano kati yenu. Unapoamua, hebu jiulize:
Unaweza kuamua kwamba ni vyema kwako kuendelea kukaa.
Ikiwa umepata majeraha, bado enenda ukapate matibabu. Sio lazima uambie mtu yeyote kiini cha majeraha zako. Lakini, ni jambo bora kumweleza daktari wako hasa ni nini kilichotendeka kwa ajili ya kupata matibabu shwari.
Unaweza kuandika madondoo au kuandika jadili kuhusu majeraha zako pamoja na nyakati ulizonyanyaswa ili baadaye ikusaidie kuamua kuondoka. Ni vizuri kuwa na mpango tayari ikiwa unahitaji kuondoka haraka iwezekanavyo.
Kurasa za kwanza za viitabu vya simu zina orodha za nambari za polisi na huduma za hatari. Ni wazo nzuri kujua nambari ya simu ya polisi iwapo tu unahitaji usaidizi wao.Wakati wa hali ya hatari, unaweza kupiga simu nambari ya 911.
Kusanya habari kama vile anwani na nambari ya simu ya watu wanaoweza kukusaidia. Ikiwezekana, weka akiba ya pesa fulani.
Jaribu kufanya vitu vinavyokufanya ujisikie vyema. Unaweza kupata ushauri au kujifunza ustadi wa kazi mpya. Watafute marafiki na familia watakaokusaidia.
Ikiwa anayekukunyanyasa angependa kubadili vitendo vyake, anaweza kupata ushauri. Kupitia kwa usaidizi wa muda mrefu, wengi wao wamejifunza kuacha vitendo vyao. Hata hivyo, ni vigumu sana kwa wale ambao wamekuwa wadhalimu hapo awali kubadilika. Unyanyasaji huendelea kuwa mbaya zaidi muda ukipitia.
Ikiwa umetoka katika hali ya kunyanyaswa, unaweza kuuliza kukaa na kuwalinda watoto wako mwenyewe.
Ikiwa unafikiri kwamba watoto wako kwenye hali ya hatari, wachukue pamoja nawe wakati unapoondoka. Tekeleza wajibu wako kwa korti mara moja ili upewe amri ya kukaa nao kisheria. Unaweza kusaidiwa na wakili. Huyu wakili wako pia anaweza kukusaidi kuuliza korti itoe amri ili baba ya watoto alipe usaidizi wa pesa kwako na za watoto. Korti itaamua juu ya chochote kilicho bora kwa watoto.
Ikiwa umepata amri ya kisheria kukaa na watoto, pengine baba yao atakuja kuwatembelea. Inapendekezwa ufanye mipango ili mtu mwingine akuwepo wakati baba yao anawachukua na kuwarudisha. Ikiwa una wasiwasi juu ya usalama ya watoto, wakili wako anaweza kuuliza korti itoe amri ili mtu mwingine asimamie matembezi haya.
Mwambie wakili ikiwa unafikiria kwamba baba ya watoto au mtu mwingine atajaribu kutoroka na watoto nje ya nchi. Ukiuliza, korti inaweza kuamuru kwamba pasi za watoto ziwekwe na korti.
Ikiwa watoto wako ni raia wa Canada, piga simu kwa Afisi ya Pasi kwa nambari 1-800-567-6868 au TTY kwa nambari 1-866-255-7655. Waulize waandike majina ya watoto kwenye orodha yao ili kwamba upigiwe simu ikiwa mtu yeyote anajaribu kuomba pasi kwa niaba yao. Ikiwa watoto wako ni raia wa nchi ingine, piga simu kwa ofisi ya ubalozi, na uwashauri kwamba wasipeane pasi kwa watoto wako.
Ikiwa una amri ya korti ya kukaa na watoto, ni wazo nzuri kuwa na nakala yako ijapo kutatokezea shida yoyote. Unaweza kupeana nakala moja kwa shule ya watoto.
Ikiwa wewe ni raia wa Canada au Mhamiaji wa Kudumu, hauwezi kuondolewa nchini Canada kama umeondoka kwenye hali ya unyanyasaji. (Mhamiaji wa Kudumu saa zingine huitwa “Landed Immigrant” kwa lugha ya kiingereza). Ikiwa haujui kama wewe ni raia au Mhamiaji wa Kudumu, piga simu kwa Ofisi ya Uraia. Angalia ndani ya kurasa za buluu iliyoko ndani ya kitabu cha simu chini ya Uraia na Uhamiaji (Citizenship and Immigration).
Ikiwa imepatikana kwamba wewe ni mkimbizi au mtu anayehitaji ulindaji, unaweza kuta maombi rasmi ili wewe binafsi uwe Mhamiaji wa Kudumu. Ikiwa wewe ni mtegemeaji wa mkimbizi au mtu anayehitaji ulindaji ambaye yuko kwenye utaratibu wa kuomba rasmi kuwa Mhamiaji wa Kudumu kwa nyote wawili, anaweza kuliondoa rasmi ombi hilo. Endapo hii imefanyika, unaweza kuomba rasmi kuwa Mhamiaji wa Kudumu chini ya sababu ya utu na huruma. Itakubidi uonyeshe waziwazi kwa nini unahitaji kuendelea kukaa nchini Canada na hakuna hakikisho kwamba utafaulu.
Ikiwa umeweka madai rasmi za kuwa wakimbizi pamoja na yule anayekunyanyasa, unaweza kuomba madai yako yatenganishwe. Madai yako yatasikilizwa tofauti na utapewa uamuzi yako binafsi.
Ni vyema upate ushauri ya kisheria. Ikiwa utalipa mtu wa kukusaidia, lazima awe ni wakili, mwanafunzi wa sheria anayesimamiwa na wakili, mwanachama wa Chambre des notaires du Québec, au mwanachama wa Jumuiya la Washauri wa Wahamiaji nchini Canada (Canadian Society of Immigration Consultants). Piga simu kwa Kituo cha Uhamiaji kilichoko karibu ili upate habari zaidi. Angalia ndani ya kurasa za buluu iliyoko ndani ya kitabu cha simu chini ya Uraia na Uhamiaji (Citizenship and Immigration).
Kama mhamiaji aliyedhaminiwa, hautaondolewa kutoka nchini Canada kwa sababu tu za shida za udhamini wako. (Angalia pia kuhusu Usaidizi wa pesa.)
Unaweza kupiga simu kwa polisi kama mwenye kukunyanyasa anakushambulia au akisema kwamba atakushambulia. Polisi wanaweza kuja kukusaidia. Maafisa wa polisi wengi wameelimishwa jinsi ya kukabiliana na unyanyasaji za familia na mahusiano mbalimbali. Wanaweza kukupeleka hospitalini ikiwa unahitaji matibabu, au wanaweza kukusaidia kwenda mahali pa usalama.
Unaweza kuenda katika kituo cha kimbilio cha wanawake iliyoko unapoishi. Hapa ni mahali pa usalama ambapo wewe na watoto wako mnaweza kukaa kwa siku au wiki kadhaa. Kulingana na rasilimali ya pesa uliyoko nazo, waweza kuulizwa kulipia baadhi ya sehemu ya malazo yako.
Wafanyikazi na wasaidizi katika kituo hicho watakupatia usaidizi na habari zaidi. Watakusaidia kupata ushauri wa sheria na usaidizi ya pesa pamoja na usaidizi juu ya mahali mapya pa kuishi ikiwa hii ni matumaini yako. Baadhi ya vitu ambayo wanavyo ni chakula, mavazi, winda na sesere ikiwa haukupata nafasi ya kukusanya vitu vyako ilipoondoka. Hawatamuelezea anayekunyanyasa mahali ulipo.
Vituo hivi vinasimamishwa na vikundi mbalimbali vya jumuiya. Nambari zao za simu kwa kawaida hupatikana kwenye kurasa za kwanza za vitabu vya nambari ya simu pamoja na nambari zingine za hatari. Unaweza pia kupiga simu katika vituo hivi ili upate ushauri makini. Sio lazima uwape jina lako.
Wakati mwingine, unaweza kuhitaji usaidizi inayohusu maslahi yako au usaidizi wa pesa. Ikiwa wewe ni mhamiaji wa kudumu au raia, una hitimu kuomba na kupata usaidizi ya maslahi pamoja na usaidizi wa pesa. Ikiwa hauhitimu, bado waweza kuomba kulingana na pale unapoishi. Mikoa na majimbo mbali mbali zina sheria tofauti za usaidizi wa pesa. Piga simu kwa ofisi kuu za mikoa au jimbo ili upate ushauri wao.
Ikiwa wewe ni Mhamiaji aliyedhaminiwa, chanzo chako cha kwanza cha usaidizi ni mdhamini wako. Lakini udhamini wako ukivunjika, unaweza kupata usaidizi kutoka kwa serikali.
Ikiwa ungali unapata usiadizi wa pesa kama Mkimbizi Anaesaidiwa na Serikali, au Mkimbizi Anayesaidiwa na Mdhamini, usaidizi wako hautakatishwa kwa sababu unaepuka kutoka kwa hali ya unyanyasaji. Aidha serikali au mdhamini wa binafsi wataendelea kulipa mahitaji yako, bora umehitimu matarajio yao. Piga simu kwa ofisi ya Kituo cha Wahamiaji Canada (Canada Immigration Centre) iliyoko karibu nawe ili ushauriwe juu ya haki zako na upate usaidizi unaohitaji.
Unapoenda kortini kupata amri rasmi ya kukaa na watoto ama kuvunja ndoa yenu, unaweza kuuliza korti iamuru baba ya watoto kulipa pesa za usaidizi kwa niaba ya watoto.
Ikiwa polisi wana mashukio yoyote kana kwamba umenyanyaswa, mwenye kukunyanyasa atashtakiwa na hatia hiyo kortini. Utahitajika kuwaeleza polisi juu ya mashtaka haya. Wanaweza kumtia ndani anayekunyanyasa wakipata ushahidi kwamba kafanya hivyo.
Ikiwa ameshikwa, anweza kukaa kwa rumande kwa masaa machache mpaka atakapopelekwa mbele ya korti ya kusikiliza dhamana. Baadaye, isipokuwa sababu nzuri ya kumweka ndani ya rumande, anaweza kuachiliwa na korti.
Ikiwa unahofia usalama wako, wafahamishe polisi kabla ya mnyanyasaji hajaachwa huru. Korti inaweza kutia masharti ya kuuachiliwa huru. Kwa mfano, korti imnaweza kumuamuru asikupigie simu au kukuona. Ikiwa hatafuata masharti haya, anaweza tena kushikwa na polisi.
Ikiwa bado unaogopa atakuumiza akiondoka kwa jela, unaweza kutafuta mahali salama pa kuishi kama makao cha kimbilio cha wanawake.
Mnyanyasasi akipatikana na hatia ya kukuumiza wewe pamoja na watoto wako, atahukumiwa na korti. Hukumu hiyo inaweza kuwa faini, muda wa majaribio, muda kwa jela au muungano ya baadhi ya hukumu hizi. Kupewa kwa hukumu ya jela au kutopewa hukumu ya jela itategemea baadhi ya mambo tofauti kama vile: kupatikana kwake kwa hatia mara ya kwanza na uzito wa madhulumu aliyofanya. Kama unahofia chochote, mfahamishe wakili wa serikali. Akihukumiwa na muda wa majaribio, korti inaweza kutia masharti za kuachiliwa kwake.
Ikiwa aliyekunyanyasa amekataa kwamba hana hatia, itakubidi wewe kutoa ushahidi kwenye jaribio lake kortini. Ushuhuda wako unaweza kutolewa nyuma ya kiwambo au kupitia mzunguko wa televisheni ukiwa kwenye chumba tofauti ndiposa usimuone aliyekunyanyasa. Pia, mtu mwingine anaweza kuwa karibu nawe unapotoa ushuhuda ili uwe na starehe.
Inaweza kuchukua muda wa miezi kadhaa kabla ya kesi kuanza. Ikiwa korti imempata na hatia aliyekunyanyasa, atahukumiwa vilivyo. Unaweza kuuliza Wakili wa Serikali kuhusu huduma za walioteswa zilizoko kwenye mkoa unapoishi ili upewe usaidizi kuhusu harakati za korti.
Ikiwa huyu aliyekukunyanyasa ni raia wa Canada hawezi kuondolewa nchini. Ikiwa yeye ni Mhamiaji wa Kudumu au mkimbizi anaweza kuondolewa nchini kama korti imempata na hatia ya kukudhulumu au hatia ayoyote ile. Amri ya kuondolewa rasmi utatolewa katika korti ya uhamiaji utakayotarishwa baada ya kupatikana kwa hatia. Hata hivyo, harakati za kutolewa inaweza kuchukua muda mrefu.
Wakati wa hatari, toka haraka iwezekanavyo. Usingoje kukusanya vitu viliyoko kwenye orodha yako – toka tu. Ukiwa na wakati, jaribu kuchukua vitu vingi viwezekanavyo. Vinaweza kuwa kama vile:
Ikiwa unafikiria kuondoka, ni wazo njema ukusanye baadhi ya vitu hivi na uviweke mahali salama, iwapo utaamua kuondoka kwa haraka.
Ni wazo njema kuumda – awali – orodha ya rasilimali ya jumuiya. Zaidi ya polisi, kuna vyama na shirika tofauti zinazoweza kukutetea na kukupa habari ya kukusaidia. Tafuta katika kurasa nyeupe, kimanjano, au kurasa za buluu kwenye kitabu ya simu upate nambari ya simu yafuatayo za shirika hizi zilizoko mjini au mkoani mwako. (Hakikisha umesasisha nambari hizi kwani hubadilika mara kwa mara.)
| Rasilimali Muhimu | Nambari ya Simu |
|---|---|
| Polisi Wanaweza kukusaidia kupima hali ya usalama na wachukua hatua dhidi ya mtu anayefanya hatia. |
(911 wakati wa hatari) |
| Vyama vya kuelimisha raia usheria Wanaweza kuweka tayari habari kwa ujumla kuhusu sheria, taratibu za sheria, na haki yako kama mteswa. |
|
| Huduma za mteswa Wanaweza kukuongoza kwa ushauri maalum na kukuambia juu ya mradi pamoja na huduma zilizoko kwa wanaodhulumishwa na hatia. |
|
| Nambari ya simu za matatizo Yanaweza kukusaidia kutatua shida wakati wa matatizo na kukuongoza kwa huduma itakayokusaidia. |
|
| Manyumba ya katikati Yanaweza kuweka tayari makao ya kimbilio, habari, na muongozo kwa wanawake walioteswa na wanyanyasi. |
|
| Ofisi za wendawazimu Pahali ambapo unaweza kupata habari au mashauri maalum kuhusu mfadhaiko, masisitizo pamoja na shida zinazosumbua akili. |
|
| Mashirika za jumuiya mbalimbali za kitamaduni na zinazotumikia wahamiaji Wanaweza kukupatia habari mahususi na kukuongoza kwa huduma za usaidizi kamili. |
|
| Ofisi ya Uraia na Uhamiaji Canada Wanaweza kujibu maswali yako kuhusu hali yako ya uhamiaji na taratibu kanuni pamoja na kukupatia habari juu ya Tekelezo ya Uhamiaji na Kulinda Wakimbizi. |
1-888-242-2100 |
| Huduma ya usaidizi wa sheria Unaweza kuhitimu kupata usaidizi wa kisheria chini ya mradi wa usaidizi wa kisheria iliyoko kwenye mkoa unapoishi bila malipo. Itakusaidia kwa familia, mambo ya uhamiaji, na haki za raia. |
|
| Watu ninaoamini Familia yako, marafiki, daktari, au washauri wa kidini wanaweza kukusaidia na kutegemewa kihisia na kwa vitu vya kawaida. |
|
| Nyingine Tafuta usaidizi zingine! Kwa mfano, unaweza kupata usaidizi kutoka kwa kitua cha wanawake iliyoko karibu nawe, kituo kinachohudumiya jumuiya na kadhalika. |